Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dansi ya asili ya kiarabu yatambuliwa na UNESCO kama urithi wa dunia

Dansi ya asili ya kiarabu yatambuliwa na UNESCO kama urithi wa dunia

Urithi wa dunia ni maeneo, majengo au mila zenye thamani kubwa ya kitamaduni au kimazingira duniani. Ni hazina inayotunzwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO ambalo huorodhesha sehemu na mila hizo na kuhakikisha zinatunzwa ipasavyo.

Mwezi Disemba mwaka 2015, UNESCO imeingiza sehemu 20 mpya katika orodha ya Urithi wa Kitamaduni, ikiwemo mila ya kunywa kahawa barazani nchini Saudia, Oman, na Qatar.

Sanaa ya asili iitwayo Al-Razfa, ambayo huchezwa hasa na wanaume Uarabuni, ni miongoni mwa urithi wa kitamaduni ambao umetambuliwa pia na UNESCO.

Kulikoni? Ungana na Priscilla Lecomte kwenye makala hii…