Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UNESCO alaani mauaji ya Ruqia Hassan mwandishi habari wa Syria

Mkuu wa UNESCO alaani mauaji ya Ruqia Hassan mwandishi habari wa Syria

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO bi Irina Bokova, ameelezea hasira yake kufuatia taarifa za kuthibitisha mauaji ya mwandishi habari wa Syria Ruqia Hassan.

Amesema analaani vikali mauaji hayo na kupongeza ujasiri wa mwandishi huyo aliyesimamia haki za binadamu na uhuru mwingine katika mazingira magumu na kupuuzia kampeni za kikatili zinazotumia itikadi kali kukandamiza uhuru binafsi wa kufikiri, kuongea na kutenda.

Mwandishi huyo wa habari na mwanaharakati Ruqia Hassan aliandika kuhusu maisha ya kila siku ya mjini Raqqa, alipokataa kuondoka wakati mji huo ulipovamiwa na Daesh. Alitekwa mwezi Julai mwaka jana na kuuawa mwezi Septemba lakini mauaji yake ndio yamethibitishwa tuu wiki hii.