Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani mashambulizi ya kigaidi Libya

Ban alaani mashambulizi ya kigaidi Libya

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon  amelaani shambulio la kigaidi nchini Libya lilolenga kituo cha polisi mjini Zliten magaharibi mwa nchi.

Taariaf iliyotolewa na msemaji wa Katibu Mkuu imesema Bwana Ban ameelezea rambirambi zake kwa familia za waliopoteza maisha au kujeruhiwa na kwa watu wa Libya.

Katibu Mkuu pia amelaani mashambulizi  yanayoendelea kutekelezwa na kundi la Daesh na washirika wake karibu na eneo liitwalo Sidra kati mwa nchi. Amelaani hatua hiyo akisema kuwa ina lengo la kupora rasilimali kutoka kwa watu wa Libya

Taarifa hiyo kadhalika imemnukuu Ban akisema kuwa vitendo hivyo ni ukumbusho kuhusu udharura wa kutekeleza makubalinao ya kisiasa na kuunda serikali ya umoja wa kitaifa  na kuongeza kwamba umoja ni njia bora kwa Walibya kukabiliana na aina zote za ugaidi.