Chanjo dhidi ya Kipindupindu sasa maradufu

Chanjo dhidi ya Kipindupindu sasa maradufu

Utolewaji wa chanjo ya kipindupindu kimataifa utaongezeka mara mbili baada ya shirika la afya ulimwenguni WHO kumtihibitisha mzalishaji wa tatu wa chanjo atakayesaidia katika upungufu na upatikanaji katika nchi nyingi .

WHO imesema kampuni hiyo ya Korea Kusini OCV imepewa jukumu la kuhakikisha kwamba  madawa na chanjo kutoka nchi mbalimbali na wakala wa kimataifa wa zabuni na mashirika kama lile la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto  UNICEF yanakidhi viwango vya, usalama na ufanisi.

Akizungumza mjini Geneva Dk Steven Martin kutoka WHO anaeleza mafanikio kutokana na hatua hii.

(SAUTI DK STEVEN)

‘‘Matokeo ya mara moja ni kwamba kwa mwaka 2016 upatikanaji wa  chanjo utaongezeka kutoka dozi milioni tatu hadi milioni sita na hii ina umuhimu katika mustakabali mathalani miaka mitatau hadi minne kwa ongezeko kubwa la uzalishaji wa chanjo .’’