Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yapongeza walioiwezesha kusaidia watu milioni moja Uganda 2015

WFP yapongeza walioiwezesha kusaidia watu milioni moja Uganda 2015

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), nchini Uganda limepongeza mataifa yaliyotoa msaada ulioliwezesha kusaidia takribani watu miolioni moja nchini humo kupata chakula mnamo mwaka wa 2015. Taarifa kamili na John Kibego.

(Taarifa ya John Kibego)

Katika taarifa yake WFP imesema, idadi ya waliofaidi kwa msaada wake iliongezeka kwa watu laki mbili ikilinganishwa na mwaka 2014.

Michael Dunford, Khaim Mkurugenzi wa WFP, nchini Uganda amesema, hali hiyo imechochewa na mmiminiko wa wakimbizi kutoka Sudan Kusini, Burundi na Jmahuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambao mpaka sasa wanakimbia mizozo nchini mwao.

Amesema kwa sasa WFP inalisha wakimbizi zaidi ya 360,000, ambayo ni idadi kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa Uganda, huku likiendelea kussaidia maelfu ya wanainchi katika eneo lenye njaa la Karamoja.

Bwana Dunford amepongeza zaidi Marekani, Kamisheni ya Ulaya, Ireland, Uingereza, Ufaransa na Marekani pamoja na wahisani binafsi wa kimataifa kwa michango yao mnamo mwaka jana.