Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bei za vyakula zimeshuka kwa mwezi Disemba:FAO

Bei za vyakula zimeshuka kwa mwezi Disemba:FAO

Shirika la chakula na kilimo FAO limesema bei za bidhaa za chakula zimeshuka kwa mwaka wa nne mfululizo mwaka jana kwa wastani wa asilimia 19.1 kutokana na kuyumba kwa uchumi kimataifa hali ambayo imechangia pia kushuka kwa bei za chuma na soko la  nishati duniani.

Kwa mujibu wa FAO miongoni mwa bidhaa zilizoathirika zaidi na kushuka kwa bei ni nyama, bidhaa zitokanazo na maziwa na nafaka , lakini pia sukari na mafuta ya mboga viliguswa.

FAO inasema uzalishaji wa bidhaa nyingi kuliko mahitaji na kuporomoka kwa thamani ya sarafu ya dola ndio sababu kubwa za kushuka kwa bei ya vyakula kwa mwaka 2015.