Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

CTBTO yaendelea kuchambua taarifa za jaribio la mlipuko DRPK

CTBTO yaendelea kuchambua taarifa za jaribio la mlipuko DRPK

Wataalamu wa Shirika la Mkataba wa Kupiga Marufuku Majaribio ya silaha za Nyuklia, CTBTO, wanaendelea na kazi ya kutathmini ripoti za mitetemo iliyobainika kwenye eneo la Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Korea, DPRK.

Katibu Mtendaji wa CTBTO Lassina Zerbo amesema hayo akihojiwa na Radio ya Umoja wa Mataifa kwa njia ya simu kutoka Ouagadougou akieleza kuwa vituo akihojiwa na Radio ya Umoja wa Mataifa amesema..

(Sauti ya Lassina)

“Kwa sasa tunafanya kazi kubaini iwapo ni mlipuko uliosababishwa kwa uhakika na binadamu au la kama ilivyotangazwa na Korea Kusini.  Kile ambacho tunaweza kufanya sasa ni kujaribu kuratibu na kuchambua taarifa hizi tulizonazo na zile zilizopatikana wakati wa majaribio ya awali yaliyofanywa na Korea Kaskazini.  Na kwa sasa zaidi ya vituo vyetu 30 vya ufuatiliaji vilipokea taarifa. Wataalamu wanaweza kupata taarifa zaidi kutoka vituo vyetu vingine. Tunahitaji angalau saa chache pengine kesho tutaweza kuwa na taarifa za kubaini aina ya mlipuko.”