Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi zinazoendelea zijitutumue kusambaza utamaduni: Dk. Kimizi

Nchi zinazoendelea zijitutumue kusambaza utamaduni: Dk. Kimizi

Nchi zinazoendelea zinapaswa kutumia mbinu mbadala ili kueneza tamaduni zao hususani katika medani ya kimataifa amesema Kaimu Katibu Mkuu wa Tume ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni(UNESCO), Dk. Moshi Kimizi.

Katika mahojiano na idhaa hii kuhusu ripoti ya hivi karibuni ya UNESCO inayoonyesha kuwa nchi zilizoendelea kiviwanda bado zimetawala katika kueneza utamaduni wao, Dk. Kimizi anataja kile ambacho kinapaswa kufanywa na nchi zinazoendelea..

(SAUTI KIMIZI)

Kuhusu upungufu wa teknolojia ambayo ni msukumo mkubwa katika kusambaza tekenolojia amesema bado fursa ipo kwani..

(SAUTI DK KIMINZI)

Agano la UNESCO kuhusu kulinda na kuendeleza tamaduni mbali mbali lilipitishwa mnamo mwaka 2005, na kuanza kutekelezwa mwaka 2007, likiwa limeridhiwa na nchi 141 na Muungano wa Ulaya kufikia sasa.