Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa polisi kuwa karibu na jamii wazinduliwa CAR

Mradi wa polisi kuwa karibu na jamii wazinduliwa CAR

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, MINUSCA umezindua mradi wa kupeleka polisi karibu zaidi na jamii kwa ushirikiano na mamlaka za usalama za nchi hiyo na zile za mji mkuu, Bangui. Priscilla Lecomte na taarifa zaidi.

(Taarifa ya Priscilla)

Kwenye taarifa iliyotolewa leo, MINUSCA imesema lengo ni kuimarisha uaminifu kati ya jamii na vikosi vya polisi na jeshi mjini Bangui, na kushirikisha zaidi jamii katika kupambana na uhalifu na ghasia mjini humo.

Kwa mujibu wa meya wa Bangui, hakuna usalama mjini humo kwa sababu ya upungufu kwa upande wa polisi huku wakiwa hawana vifaa na uelewa wa kutosha wa kutekeleza majukumu yao.

Mradi huo unaofadhiliwa na MINUSCA unalenga kuanzisha kampeni ya kuelimisha jamii kuhusu majukumu ya polisi na kuunda baraza litakalounganisha wawakilishi wa polisi na jamii katika vitongoji nane vya Bangui.