Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMA yalaani mashambulio ya Taliban Kabul yaliouwa 5 na kujeruhi 56

UNAMA yalaani mashambulio ya Taliban Kabul yaliouwa 5 na kujeruhi 56

Mpango wa Umoja wa Mataifa wa msaada nchini Afghanistan UNAMA umelaani mashambulio ya mabomu katika maeneo ya raia mjini Kabul mapema mwezi huu.

Kundi la Taliban limekiri kuhusika na mashambulio matatu tofauti ya kujitoa muhanga yaliyofanyika kati ya tarehe mosi na 4 Januari amvbayo yamekatili maisha ya watu watano na kujeruhi wengine 56.

Waaathitika hao ni pamoja na watoto 10 na wanawake 9 waliouawa au kujeruhiwa wakiwa katika mihangaiko ya maisha ya kiloa siku majumbani kwao, kwenye migahawa, madukani, maofisini au wakisafiri mitaani. Pia wafanyakazi wane wa kiraia wa Umoja wa Mataifa ni miongoni mwa waliojeruhiwa.

Kwa mujibu wa UNAMA siku yam waka mpya Taliban ilishambulia mgahawa wa Jardin na kuuwa watu wawili na kujeruhi wengine 18 wakati mashambulio mawili ya kujitoa muhanga yaliyotekelezwa na Taliban tarehe 4 Januari karibu na uwanja wa ndege wa Kabul yalikatili maisha ya watu watatu na kujeruhi wengine 38.