Jaribio la bomu la Haidrojeni DPRK ni ukiukwaji wa azimio la Baraza la Usalama:IAEA

6 Januari 2016

Serikali ya Jamhuri ya watu wa Korea DPRK leo Jumatano imetangaza kwamba imefanya jaribio la bomu la Haidrojeni.

Akizungumzia tamko hilo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki , IAEA Bwana Yukiya Amano amesema..

(SAUTI YA YUKIYA AMANO)

"Endapo itathibitika ni kweli jaribio hilo limefanyika basi huo ni ukiukwaji mkubwa wa azimio la Baraza la Usalama na ni wa kusikitisha. Ninawahimiza sana DPRK kutekeleza kikamilifu maazimio ya baraza la usalama na IAEA."

Ameongeza kuwa IAEA iko tayari kusaidia kwa njia ya amani suluhu ya masuala ya nyuklia ya DPRK kwa kuanza kuthibitisha shughuli zake za nyuklia baada ya muafaka kufikiwa baina ya nchi husika.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud