Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aelezea wasiwasi wake kuhusu hali ya kisiasa inayoendelea Haiti:

Ban aelezea wasiwasi wake kuhusu hali ya kisiasa inayoendelea Haiti:

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameelezea wasiwasi wake kuhusu hali ya kisiasa nchini Haiti inayoambatana na mchakato wa uchaguzi.

Ameutaka uongozi wa Haiti na wadau wote wa kisiasa kutatua changamoto zilizopo na kuhakikisha kwamba mchakato wa uchaguzi unakamilika haraka iwezekanavyo katika njia ya uwazi, jumuishi nay a haki.

Katibu Mkuu anatambua kwamba tangu Januari 2015 bunge la nchi hiyo halifanyi kazi , na kwa mantiki hiyo amesisitiza umuhimu wa wa kuapishwa kwa bunge jipya kwa mujibu wa muda uliowekwa na katiba ili kuhakikisha kwamba kurejea kwa taasisi kidemokrasia na kurejesha tena utulivu wa kisiasa kisiwani humo.