Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Changamoto ya Mediterenea ni miongoni mwa maafa ya kibinadamu:Swing

Changamoto ya Mediterenea ni miongoni mwa maafa ya kibinadamu:Swing

Mkuu wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM Lacy Swing amesema wakati idadi kubwa ya wahamiaji na wakimbizi waliowasili barani Ulaya mwaka 2015 imeongeza shinikizo na hofu, hiyo sio changamoto iliyo nje ya uwezo wa bara Ulaya kama muungano kuishughulikia kwa pamoja.

Amesema kunahitajika fikra thabiti, za pamoja na hatua ili kuweza kuwa na mtazamo madhubuti wa suala hilo.

Ameongeza kuwa hivi sasa kuna watu milioni 60 duniani ambao wametawanywa kutokana na kukimbia mauaji, vita, migogoro au majanga, ambayo ni idadi kubwa kabisa tangu vita vya pili vya dunia ambapo wakati huo watu walikuwa wakikimbia Ulaya na sasa ni zamu yao kupokea wanaokimbia.

Kwa mujibu wa takwimu za IOM Zaidi ya wakimbizi, wahamiaji na waomba hifadhi 900,000 wamewasili kupitia Mediteranea hadi Ugiriki na Italia, huku wengine 3500 wakipoteza maisha yao.