Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MONUSCO yasaidia kujenga kituo cha Redio na hospitali

MONUSCO yasaidia kujenga kituo cha Redio na hospitali

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC MONUSCO, umefungua leo rasmi jengo la kituo cha redio ya kijamii katika mji wa Mpiana, yapata kilomita 95 kusini mwa kituo cha Manono, Tanganyika, zamani kikiitwa Katanga.

Ujenzi wa jengo hilo ulifadhiliwa na MONUSCO, na uligharimu zaidi ya dola 25,000 za Kimarekani.

Wakati huohuo, MONUSCO imesaidia kujenga kituo cha matibabu katika gereza kuu la mji wa Goma, mashariki mwa DRC. Patrick Mukendi ni Mkurugenzi wa gereza kuu la Goma, na anaelezea manufaa ya kituo hicho katika gereza hilo.

(Sauti ya Patrick Mukendi)

Ni  mamlaka ya gereza ndio ilifikiria kuboresha hali za mahabusu katika gereza kuu la Goma kwa kupanua kituo cha tiba cha mahabusu. Jengo hili linalenga kupunguz msongamano katika kliniki ambayo ilikuwa na uwezo mdogo wa kuhudumia wafungwa wetu wagonjwa. Linajumuisha chumba cha matibabu chenye vitanda vinane, sehemu ya dawa , choo na bafu.”