Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yahitaji dola milioni 80 kushughulikia mahitaji ya kibinadamu Sudan Kusini:

IOM yahitaji dola milioni 80 kushughulikia mahitaji ya kibinadamu Sudan Kusini:

Ikiwa ni mzaidi ya miaka miwili tangu kuzuka mgogoro wa Sudan Kusini mahitaji ya kibinadamu nchini humo yanasalia kuwa makubwa saana kwa mujibu wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM ambalo sasa linahitaji dola milioni 80.2 ili kutoa msaada wa kuokoa maisha kwa maelfu ya watu. Flora Nducha na taarifa kamili.

(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)

Ghasia, kutokuwepo fursa za kuwafikia waathirika na usalama mdogo wa chakula vinaendelea kuongeza mahitaji na kuwa chachu ya maelfu kuw wakimbizi wa ndani. Mwezi Septe,bam waka jana asilimia 34 ya watu wote nchini humo walikabiliwa na ukosefu wa chakula ikiwa ni asilimia 80 zaidi yam waka 2014.

Takriban watu milioni 2.3 wamezikimbia nyumba zao tangu kuanza kwa machafuko wakiwemo milioni 1.66 waliosalia kuwa wakimbizi wa ndani huku wengine 647,800 wakikimbilia nchi jirani.

Kwa mujibu wa IOM mwaka 2016 mahitaji yataongezeka Sudan Kusini huku vita vikiendelea na maelfu bado wanakimbia nyumba zao.Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa watu milioni 6.1 watahitaji msaada wa kibinadamu Sudan Kusini 2016 ikiwemo afya, malazi,usafi na  maji safi na salama.