Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM walaani mashambulio dhidi ya misikiti Babylon Iraq

UM walaani mashambulio dhidi ya misikiti Babylon Iraq

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa nchini Iraq Ján Kubiš, amelaani mashambulio yaliyofanyika dhidi ya misikiti mitatu ya Kisuni kwenye jimbo la Babylon usiku wa kuamkia leo na vitendo vingine vya ghasia.

Mashambulio hayo matatu ni jarikbio la kuongeza mvutano nchini Iraq na kwenye ukanda mzima amesema bwana Kubiš.Akiongeza kwamba walioendesha mashambulizi hayo wanajaribu kutumia hali ya sasa ya kikanda na kudhoofisha umoja wa Iraq na watu wake na wanatimiza matakwa ya magaidi wa ISIL.

Wakati huohuo amerejelea wito uliotolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon wa kudumisha utulivu na kujizuia kuchukua hatua zozote kufuatia kunyongwa kwa Sheikh Nimr al-Nimr na kuwataka viongozi wote wa kikanda kushirikiana na kuepuka kuendelea Zaidi kwa mvutano wa kidini. Ban amefadhaishwa na kitendo cha Saudia kuwanyoka kuwanyoka watu 47 akiwemo Sheikh Nimr al-Nimr.