Ban amezungumza kwa simu na mawaziri wa mambo ya nje wa Iran na Saudia

4 Januari 2016

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amezungumza kwa njia ya simu na waziri wa mambo ya nje wa Saudia Abel bin Ahmed Al-Jubeir, na waziri wa mambo ya nje wa Iran Mohammad Javad Zarif.

Akizungumzana Bwana Zarif, Ban amerejea kauli yake kuhusu mauaji ya Sheikh al-Nimr na wafungwa wengine 46 yaliyotekelezwa na serikali ya Saudia Januari pili mwaka huu. Pia amezungumzia kulaani kwake vikali shambulizi dhidi ya ubalozi wa Saudia mjini Tehran na amemtaka waziri huyo wa mambo ye nje kuchukua hatua zinazohitajika kulinda maeneo ya kidplomasia nchini humo.

Na alipozungumza na waziri Al-Jubeir, tKatibu Mkuu amerejelea msimamo wake kuhusu hukumu ya kifo na kusikitishwa na mauaji ya Sheikh al-Nimr, ambaye kesi yake alishaizungumza kwa uongozi wa Saudia mara kadhaa.

Ban amesema mashambulizi dhidi ya ubalozi wa Saudia inasikitisha lakini akaongeza kuwa tangazo la kuvunja uhusiano wa kibalozi baina ya Saudia na Tehran ni suala linalotia hofu. Na kuhusu Yemen Ban ameutaka uongozi wa Saudia kutathimini upya ahadi yake ya kusitisha mapigano.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter