Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwakilishi maalumu wa UM kwa Palestina ajiuzulu

Mwakilishi maalumu wa UM kwa Palestina ajiuzulu

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa kuhusu haki za binadamu kwa eneo linalokaliwa la Palestina Makarim Wibisono, leo amewasilisha barua yake ya kujiuzulu rasmi kuanzia tareje 31 Machi 2016, kwa Rais wa baraza la haki za binadamu.

Mtaalamu huyo huru ameelezea masikitiko yake kwamba wakati wote alioshika wadhifa huo Israel imeshindwa kumpa fursa ya kwenda kwenye eneo la Palestina linalokaliwa. Ameongeza kuwa kwa bahati mbaya juhudi zake za kutaka kuboresha maisha ya Wapalestina walio wahanga wa ukiukwaji wa haki za binadamu katika eneo hilo linalokaliwa zimegonga mwamba kila alipojaribu.

Mwakilishi huyo amesema alipochukua madaraka mwezi Juni 2014 alihakikishiwa kwamba atapata fursa ya kufika kwenye eneo la Palestina linalokaliwa, lakini matokeo yake maombi yote ya mdomo na aliyoandikwa yote hayakuzaa matunda.