Msaada wa washirika ni muhimu katika kufanikisha wajibu wa UNAMA

4 Januari 2016

Mpango wa Umoja wa mataifa nchini Afghanistan UNAMA umesema unatambua na kuwashukuru washirika wake kwa msaada mkubwa nchini humo mwaka 2015. Kauli hiyo imetolewa kwenye hafla maalumu iliyofanyika mjini Kandahar kusini mwa nchi hiyo.

Wajumbe 17 wa mashirika ya kijamii wakiwemo wawakilishi wa jumuiya za kiraia vyombo vya habari, vijana, makundi ya haki za wanawake,, maafisa wa kamati ya Amani ya Kandahar na maafisa wa serikali waliunga na wafanyakazi wa UNAMA katika hafla hiyo.

Kwa mujibu wa Simon Hermes mkuu wa UNAMA Kandahar maelfu ya watu kwenye jimbo la Kandahar waliweza kufikiwa mwaka 2015 huku wakichagizwa kuhusu haki za binadamu, haki za wanawake, amani na maridhiano, utawala wa sheria na masuala mengine muhimu.

UNAMA ilianzishwa na baraza la usalama mwaka 2002 kwa ombi maalumu la serikali ya Afghanistan.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter