Martin Kobler atuma salamu za mwaka mpya kwa Walibya

2 Januari 2016

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya Martin Kobler, ametuma salamu zake za mwaka mpya kwa raia wa Libya akiwatakia amani, matumaini na ukuaji wa uchumi.

Kwenye ujumbe wake uliotolewa tarehe mosi Januari, Bwana Kobler amesema ingawa mwaka wa 2015 haukuwa na baraka kwa Libya, makubaliano ya kisiasa yaliyosainiwa mwisho wa mwaka yameleta matumani, akiongeza kwamba mwaka 2016 utakuwa mwaka wenye fursa ya kukomesha mzozo wa Libya na kujenga upya amani na umoja wa nchi.

Aidha Bwana Kobler amewaomba Walibya wote waunge mkono makubaliano ya kisiasa na serikali ya muafaka.

Akikariri msimamo wake wa kusaidia mchakato wa amani unaoongozwa na Walibya, amesema kwamba Umoja wa Mataifa utaendelea kusaidia Libya katika jitihada zake za kutatufa amani na maridhiano. 

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter