Skip to main content

Ban ampongeza waziri mkuu wa Iraq kwa vita dhidi ya ISIL

Ban ampongeza waziri mkuu wa Iraq kwa vita dhidi ya ISIL

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-Moon leo amempigia simu waziri mkuu wa Iraq Haider al-Abadi, na kumpongeza kwa mafanikio ya vikosi vya usalama vya Iraq kwa vita dhidi ya kundi la kigaidi la ISIL.

Ban pia amebainisha kuwa ukombozi wa Ramadi ni ushindi mkubwa na kusisitiza haja ya kuchukuliwa hatua za kurejesha utawala wa sheria halikadhalika huduma muhimu mjini Ramadi ili kuruhusu wakimbizi wa ndani kuweza kurejea haraka iwezekanavyo.

Ban pia amesema Umoja wa Mataifa uko tayari kusaidia katika suala hilo.Hata hivyo ameelezea hofu yake kuhusu vitendo vya utekaji nyara vya karibuni dhidi ya kundi la raia wa Qatari nchini humo wakiwemo watoto.

Amemtaka waziri mkuu kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha watu hao wanaachiwa mara moja na wakiwa salama.