Skip to main content

Rais wa Burundi apinga vikosi vya AU kuingia nchini mwake:

Rais wa Burundi apinga vikosi vya AU kuingia nchini mwake:

Rais wa Burundi ametupilia mbali mpngo wa Muungano wa Afrika wa kutuma vikosi vya walindamamani nchini mwake. Kiongozi amesema vikosi ikiwa vitaingia Burundi bila idhani ya serikali, vitachukulia kuwa bi majeshi ya uvamizi na serikali yake iko tayari kupambana nao. Ameyasema hayo hii leo akiyajibu maswali ya wananchi redioni katika kipindi cha moja kwa moja.Kutoka Bujumbura, muandishi wetu wa maziwa makuu Ramadhani KIBUGA anaripoti.

(TAARIFA YA RAMADHAN KIBUGA)

Akiulizwa na wananchi swali hilo la kuletwa vikosi vya walindamani kwenye kipindi cha moja kwa moja redioni kupitia njia ya simu, Rais wa Burundi Pierre NKURUNZIZA amefahaamisha kuwa Kwa mujibu wa sheria ya nchi hii , kwanza vikosi hivyo vinaombwa na serikali , kitu ambacho hakikufanywa au serikali kushauriwa , pili amesema Rais Nkurunziza vikosi vinatumwa kama hamna serikali kama ilivokuwa Somalia au Jamuhuri ya Afrika ya kati na hiyo sio hali halisi ya Burundi, tatu ameongeza Rais Nkur vikosi vinakuja kama kuna makundi yanahasimiana na wakaafikiana kutumwa vikosi hivo.

Rais Pierre Nkurunziza amesema vikosi vivyo vikiingia Burundi vitachukuliwa kuwa ni uvamizi na taifa halitalea mikono.

(SAUTI YA

“ Burundi ni taifa huru, hata katika azimio la umoja wa mataifa la mwezi uliopita katika hatua walizochukua hamna sehemu wanasema vikosi vya kimataifa vitaletwa Burundi , tena huwezi kuleta vikosi vya walindamana bila idhni ya baraza la usalama la umoja wa mataifa. Azimio lilikuwa wazi kwanzba ni lazima mataifa yazingatie uhuru na enzi vya burundi, sasa kama watakuja kwa kupuuza hatua hizo, watakuwa wameishanmbulia Burundi, kila mrumdi atasimama awapige vita. Nchi itakuwa imevamia, kama hali ni hiyo tutajihami. “Aidha kwenye kipindi hicho, Rais Nkurunzizaa amekosoa vikali utaratibu wa maandalizi ya mazungumzo yaliyofanyika wiki hii nchini Uganda hasa kwa kukailika kundi alolitaja kuwa halitambuliki ki sheria akimaanisha wapinzani wanaojumuika Muungano wa vyama vya kisiasa na mashirika ya kiraia yaliyopinga muhula wake tatu kwenye uongozi wa nchi.

Tayari serikali ilitishia kutoendelea na mazungumzo hayo ambayo yataitishwa tarehe 6 january mwakani mjini Arusha, ikiwa kundi hilo la wapinzani litaalikwa.

Hayo ni wakati Muungano wa Afrika umetishia kuchukua vikwazo kwa upande wowote utakaothubutu kususia mazungumzo yajayo ya Arusha.