Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya wakimbizi na wahamiaji milioni 1 wamewasili Ulaya 2015 kupitia bahari:UNHCR

Zaidi ya wakimbizi na wahamiaji milioni 1 wamewasili Ulaya 2015 kupitia bahari:UNHCR

Zaidi ya wakimbizi na wahamiaji milioni moja wamekimbilia Ulaya mwaka huu kwa njia ya bahari limesema shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR.

Wengi wa watu hao wamewasili Ugiriki na Italia, wengi wao wakitumia njia hatari ya boti zinazomilikiwa na wasafirishaji haramu wa watu. Karibu nusu milioni ya watu hao wametumia bahari ya Mediteranean na hususan kutoka Syria ambako vita bado vimechacha, huku asilimia 20 wakiwa ni kutoka Afghanistan na asilimia 7 kutoka Iraq.

Lakini cha kusikitisha Zaidi ni idadi ambayo UNHCR inasema hawajulikani waliko wakidhaniwa kuwa wamekufa maji. Mwaka 2015 pekee ni 3,700. Mbali ya wanaosafiri majini takwimu za karibuni zinaonyesha wengine 34,000 wamevuka mpaka kutoka uturuki na kuingia Bulgaria na Ugiriki kutumia nchi kavu.