Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kwaherini Somalia, tumepiga hatua katika utulivu: Kay

Kwaherini Somalia, tumepiga hatua katika utulivu: Kay

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Balozi Nicholas Kay amemaliza muda wake  na hivyo kuagwa rasmi katika hafla fupi  iliyofanyika katika uwanja wa ndege wa Aden Abdulle, muda mfupi kabla ya kurejea nyumani Uingereza.

Akiongea wakati akiwaaga Wasomalia na jumuiya ya kimataifa katika hafla hiyo,  Balozi Kay aliyetumikia nafasi hiyo kwa miaka miwili  amesema anaiacha Somalia yenye hatua nzuri kuelekea amani  ikilinganishwa na miaka iliyopita.

(SAUTI KAY)

‘‘Leo nafikiri ni siku ya furaha na chanya kadhalika, nina furaha kwasababu kwanza naenda nyumbani, na naungana na familia yangu. Nafikiri tunaweza kuona hakika kwamba Somalia kuna kasi isiyozuilika ya kuelekea amani, utulivu, mafanikio na demokrasia na kasi hiyo haikuwepo miaka mitatau iliyopita.’’

Shamrashamra na undani zaidi wa hafla ya kumuaga mwakilishi huyo wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Balozi Nicholas Kay aliyerejea nyumbani  nchini Uingereza zitakujia katika makala zetu motomoto.