Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchaguzi waendelea kwa amani CAR

Uchaguzi waendelea kwa amani CAR

Uchaguzi wa rais na wabunge unaendelea kwa amani na utulivu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, huku waangalizi wakiripoti kwamba watu wamejitokeza kwa wingi kwa ajili ya kupiga kura. Taarifa zaidi na Flora Nducha.

(Taarifa ya Flora Nducha)

Hii ni kwa mujibu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MINUSCA, ambao umeshiriki katika kuhakikishia usalama wa mchakato huo pamoja na vikosi vya polisi vya kitaifa.

Kamanda wa Vikosi vya MINUSCA Jenerali Bala Keita ameongea na redio Guira FM ya MINUSCA wakati akizuru vituo vya kupiga kura mjini Bangui.

(Sauti ya Bwana Keita)

« Kila kitu kimepangwa vizuri. Watu wamepanga mstari. Inaonekena kwamba kila kitu kinaendelea vizuri. Nadhani kwamba saa kumi na moja na nusu, watu wote watakuwa wamepata fursa ya kupiga kura, na tutaanza kuhesabu kura saa kumi na mbili.”

Awamu ya pili ya uchaguzi wa rais itafanyika tarehe 31 mwezi Januari, mwaka 2016.