Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa CAR watamani maridhiano

Wakimbizi wa CAR watamani maridhiano

Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, zaidi ya watu 400,000 wamelazimika kuhama makwao tangu kuanza kwa mzozo nchini humo miaka miwili iliyopita.

Miongoni mwao, watu wapatao 100,000 wametafuta hifadhi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, wakivuka mto wa Ubangui na kupatiwa hifadhi kwenye kambi kupitia misaada ya Shirika la Umoja wa MAtaifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR, serikali na wadau mbalimbali.

Lakini hadi ukimbizini, bado sintofahamu imeendelea baina ya jamii ya wakristo na waislamu.

Ungana na Priscilla Lecomte kwenye makala hii.