Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bado kipindupindu tatizo Tanzania: Dk Azma

Bado kipindupindu tatizo Tanzania: Dk Azma

Licha ya juhudi za wadau wa kimataifa na serikali, ugonjwa wa kipindupindu bado umeendelea kuuwa watu wengi nchini Tanzania amesema mtaalamu wa afya ya jamii ya epodemiolojia Dk Azma Simba kutoka wizara ya afya.

Katika mahojiano na idhaa hii Dk Azma amesema licha ya kwamba kwa baadhi ya mikoa mlipuko wa kipindupindu unadhibitiwa lakini kwa ujumla ugonjwa unasambaa kwa kasi ambapo zaidi ya watu 12,000 wameathirika.

(SAUTI DK AZMA)

Kadhalika amesema kile anachokiona kinakwamisha kutokomeza kwa kasi kipindipindu Tanzania.

(SAUTI DK AZMA)

Takribani watu 200 wamefariki dunia kutokana na mlipuko wa kipindupindu nchini Tanzania ambao ulianza mnamo Agosti 15, 2015.