Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelfu ya raia wa Sudan wanakimbilia Sudan Kusini kusaka usalama:UNHCR

Maelfu ya raia wa Sudan wanakimbilia Sudan Kusini kusaka usalama:UNHCR

Maelfu ya raia wa Sudan wamekuwa wakimbilia Sudan Kuisni kutafuta usalama kwa mujibu wa shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR.

Miongoni mwao ni Amal Bakith na watoto wake ambao wamesafirishwa na basi la UNHCR kuelekea kambi ya Thok Sudan Kusini. Kwao imekuwa ni faraja ikilinganishwa na Sudan walikotoka ambako mapigano yamemfanya mama yao mkulima kushindwa kupanda chakula chochote.

UNHCR inasema makubaliano ya amani ya August 2015 yaliyopaswa kukomesha mapigano yamekuwa yakikiukwa na mustakhbali wake sasa uko njia panda.

Serikali ya Juba imefungua milango yake kwa wale wanaokimbia miaka minne ya vita Sudan, na kutenga eneo maalumu kwa ajili ya makazi ya maelfu ya wakimbizi hao.

Mapigano wanayokimbia baina ya serikali ya Sudan na majeshi ya upinzani kwenye milima ya Nuba na jimbo la Kordofan Kusini huchacha wakati wa mwisho wa mwaka mvua zinapomalizika.