Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi mdogo umebadili maisha ya walemavu karibu 500 nchini Mali: MINUSMA

Mradi mdogo umebadili maisha ya walemavu karibu 500 nchini Mali: MINUSMA

Nchini Mali, mzozo umeathiri sana jamii hasa kaskazini mwa nchi. Moja ya majukumu ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo MINUSMA ni kurejesha ukuaji wa uchumi na kusaidia vikundi vya jamii vinavyoteseka zaidi, kwa mfano watu wenye ulemavu.

Kupitia mpango unaoitwa Miradi yenye mafanikio ya haraka yaani Projets à Impact Rapide, MINUSMA inafadhili miradi midogo midogo kwenye miji ya kaskazini mwa Mali. Utengenezaji wa sabuni ni moja ya miradi hiyo inayosaidia watu wenye ulemavu. Mradi huo umeanzishwa mwezi Oktoba mwaka 2014 na umenufaisha watu karibu 500. Kulikoni? Ungana na Amina Hassan kwenye makala hii.