Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Raia wa Kunduz Afghanistan wapata msaada wa kibinadamu

Raia wa Kunduz Afghanistan wapata msaada wa kibinadamu

Zaidi ya familia 100 zilizoathiriwa na mapigano kwenye eneo la Kunduz, nchini Afghanistan, zimepatiwa misaada ya kibinadamu kutoka kwa Umoja wa Mataifa na wadau wake.

Hii ni kwa mujibu wa Ujumbe was Umoja wa Mataifa nchini humo, UNAMA, ukisema kwamba familia hizo zimepokea vyakula na vifaa mbalimbali, zikiwemo shuka na ndoo za maji.

Kwa ujumla ni familia zaidi ya 500 zilizosaidiwa tangu mwezi Septemba wakati mashambulizi ya waasi wa Taliban yalipoanza. Raia karibu 300 wameuawa na wengine 550 kujeruhiwa wakati wa mapigano hayo kati ya Wataliban na jeshi la serikali.