Ban akaribisha muafaka wa Japan na Korea kuhusu wanawake waliotumika kama faraja wakati wa vita kuu:

28 Disemba 2015

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amekaribisha muafaka wa serikali za Japan na Jamhuri ya Korea kuhusu masuala yahusuyo wanawake waliotumiwa kingono kama faraja kwa askari wa Japan wakati wa vita kuu ya pili ya dunia.

Muafaka huo umefikiwa Jumatatu kwenye mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje mjini Seoul. Katibu Mkuu anatumai kwamba makubalino hayo yatasaidia kuimarisha uhusiano baiana ya mataifa hayo mawili.

Amepongeza mtazamo na uongozi wa Rais Park Geun-hye wa Jamhuri ya Korea na waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe kwa nia ya kuboresha uhusiano wa baadaye.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud