Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Gambia yapiga marufuku ukeketaji

Gambia yapiga marufuku ukeketaji

Mapambano dhidi ya ukekeketaji yamechukua sura mpya barani Afrika kufuatia taifa la Gambia kupitisha sheria ya kupiga marufuku vitendo hivyo nchini humo. Joshua Mmali ana maelezo kamili.

(TAARIFA YA JOSHUA)

Hatua hiyo imepokelewa vyema na Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu(UNFPA) ambapo kupitia mtandao wake wa kijamii wa twitter limeandika kuwa sheria hiyo ya kupiga marufuku ukeketaji imepitishwa na bunge la nchi hiyo mchana huu.

Katika hatua nyingine UNFPA kwa kushirikiana na gazeti la Guardian, wametangaza tuzo za waandishi wa habari barani Afrika wanaoripoti masuala ya ukeketeji ikiwa ni juhudi za kusongesha harakati dhidi ya vitendo hivyo vinavyokwenda kinyume na haki za binadamu .

Kwa mujibu wa taarifa ya UNFPA, tuzo hiyo ilitangazwa rasmi na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon wakati akiwa ziarani nchini Kenya mwezi Oktoba.

Shirika hilo limesema kuwa lengo ni kuongeza uweelewa wa jamii kuhusu ukeketaji barani Afrika kupitia vyombo vya habari na kuongeza kuwa mshindi wa jumla atajipatia fursa ya mafunzo katika ofisi ya Guarina jijini London, Uingereza.