Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pande zote Syria zapaswa kujali maslahi ya raia wake: Demistura

Pande zote Syria zapaswa kujali maslahi ya raia wake: Demistura

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa , kwa kauli moja lilipitisha hapo tarehe 18 Desemba 2015, zaidi ya azimio 2254 (2015) , kwamba mjumbe maalumu wa Umoja wa mataifa kwa Syria, Mheshimiwa Staffan de Mistura, ameongeza juhudi za kuwaleta pamoja wawakilishi wa Serikali ya Syria na wigompana wa upande wa upinzani na wengineo kushiriki katika mchakato wa kisiasa kuelekea utekelezaji wa malengo na kanuni za ufumbuzi wa kisiasa kwa mgogoro wa Syria, kama zilivyoainishwa katika katika tamko la Geneva la 30 Juni 2012, na taarifa ya Vienna ya Oktoba 30 na Novemba 14, 2015.

Kwa mujibu wa yaliyoainishwa kwenye azimio mwakilishi huyo maalumu anampango wa kukamilisha majadiliano yake mapema mwezi Januari kwa mtazamo wa kuanzisha mazungumzo ya ndani ya Syria mnamo Januari 25 mwaka 2016 mjini Geneva.

Anatumai kupata ushirikiano wa pande zote husika nchini Syria katika mchakato huu lakini pia anatambua umuhimu kundi la kimataifa linalounga mkono Syria.

Demistura amesema watu wa Syria wameteseka vya kutosha na janga lao limesambaa pia katika nchi jirani n ahata mbali zaidi, hivyo wanastahili kuonyeshwa kuwa pande zote husika nchini mwao zinajali maisha yao na maslahi yao. Pande hizo zinapaswa kuonyesha uongozi shupavu, na mtazamo thabiti kwa kuweka kando tofauti zao kwa manufaa ya Wasyria.