WHO yapeleka masaada wa madawa kwa watu milioni 1.2 Taiz Yemen

28 Disemba 2015

Shirika la afya duniani WHO mwishoni mwa wiki limepeleka Zaidi ya tani 100 za madawa na vifaa ya tiba kwa watu Zaidi ya milioni moja kwenye wilaya 8 za jimbo la Taiz nchini Yemen ambako watu takribani milioni 3 wakiwemo wakimbizi wa ndani 329,00 wanahitaji haraka msaada wa kibinadamu. Priscilla Lecomte na taarifa kamili.

(TAARIFA YA PRISCILLA)

Msaada huo ambao ulipelekwa mara baada ya kutangazwa usijitishwaji mapigano ni pamoja mitungi ya gesi ya oxygen, mashine za kufanyia vipimo na vifaa vya upasuaji, na mitambo ya huduma za dharursa. Vifaa hivyo vimegawanywa katika hospitali na vituo vya afya 13.

Kwa mujibu wa WHO hali ya afya imeendelea kuzorota Taiz wakikabiliwa na upungufu wa wahudumu wa afya, , madawa na mafuta, pamoja na fursa finyu kwa jumuiya ya kimataifa ya kugawa misaada kutokana na matatizo ya kiusalama yaliyochangia pia vituo vingi vya afya kufungwa.

WHO imetoa wito kwa pande zote kuhakikisha kwamba misaada ya kibinadamu inaingizwa bila masharti yoyote na pia kuwaruhusu wahudumu wa afya kuwafikia waathirika.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter