Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kobler awapongeza raia wa Libya kutimiza miaka 64 ya Uhuru

Kobler awapongeza raia wa Libya kutimiza miaka 64 ya Uhuru

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa kwa ajili ya Libya Martin Kobler amewapongeza raia wa Libya kwa kuadhimisha miaka 64 tangu kujinyakulia uhuru wake.

Pamoja na changamoto zinazoikabili nchi hiyo leo, Libya imebakia nchi huru na taifa lenye uadilifu tangu 1951. Na kuongeza kuwa bkuna mengi ya kujifunza tangu kuzaliwa kwa taifa hilo.

Leo ni wiki moja tangu kutiwa saini muafaka wa kisiasa wa Libya ambao unairejesha nchi hiyio katika njia ya kujenga taifa la kisasa la kidemokrasia .Amewachagiza Walibya wote kuungana kuunga mkono taasisi za serikali jumuishi.

Amesema itakuwa muhimu taiafa hilo kusherehekea miaka 65 hapo mwakani kama taifa huru lenye mshikamano.