Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ufadhili kwa UM unapungua huku mahitaji yakiongezeka: Ban

Ufadhili kwa UM unapungua huku mahitaji yakiongezeka: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-Moon amesema ufadhili kwa Umoja wa mataifa unaendelea kupungua wakati mahitaji ykiendelea kuongezeka nah ii ni changamoto lakini Umoja wa mastaifa unafanya kila liwezekanalo kutekeleza majukumu yake kwa mahitaji ya dunia na kwa bajeti iliyopo kwa kutumia ubunifu na kufanya kazi kwa bidi. Amina Hassan na taarifa kamili.

(TAARIFA YA AMINA HASSAN)

Akizungumza baada ya baraza kuu kupitisha bajeti yam waka 2016-2017 amesema bajeti hiyo inadhihirisha changamoto za kifedha zinazoikabili dunia kwa miaka kadhaa sasa. Bajeti hiyo imeongeza fedha katika kuhakikisha malengo ya maendeleo endelevu (SDGS) yanafikiwa lakini imepunguza rasilimali kwa idara ya habari kwa umma na hili Ban amesema litatoa changamoto ingawa Umoja wa mataifa umejidhatiti kuhakikisha malengo na majukumu yake yanatekelezwa. Ameongeza kuwa mwaka 2015 ulikuwa na changamoto nyingi kwenye agenda ya kimataifa lakini

(SAUTI YA BAN)

“Wakati huohuo tunaweza kujivunia mafanikio makubwa tuliyokamilisha hususani Addis Ababa ajenda ya ufadhili kwa ajili ya maendeleo ,ajenda yam waka 2030 ya maendeleo endelevu na makubaliano ya Paris kwa ajili ya mabadiliko ya tabia nchi, haya na mengine yanadhihirisha kwamba ushirikiano wa kimataifa unafanya kazi”

Amesema mwaka 2016 Umoja wa Mataifa utachukua hatua juu ya miapango yake kwa afya Zaidi na Amani duniani ambapo watu wote wanapswa kuishi kwa hadhi inayostahili.