Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania haina polio tena, siri ni kuwasaka wagonjwa kila kona: Dk Mbando

Tanzania haina polio tena, siri ni kuwasaka wagonjwa kila kona: Dk Mbando

Baada ya safari ya muda mrefu ya kukabiliana na ugonjwa wa Polio unaosababisha kupooza kwa viungo vya mwili, Tanzani hatimaye imetngazwa kuwa imefanikiwa kutokomeza ugonjwa huo.

Tangazo hilo lililotolewa na mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa, lile la afya ulimwenguni WHO, pamoja na la kuhudumia watoto UNICEF, linalezwa kuwa ni juhudi za pamoja za wizara ya afaya ya nchi hiyo na wadau wa afya.

Katika mahojiano maaluma na Jospeh Msami wa idhaa hii, Katibu Mkuu wa Katibu Mkuu wa wizara ya afya Tanzania Dk Donan Mbando anasema siri ni kampeni maalum ikiwa ni mwitikio wa makubaliano ya kimataifa. Kwanza anaeleza tangazo hili lina maana gani katika mustakabali mzima wa afya Tanzania.

(SAUTI MAHOJIANO)