Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahamat Saleh Annafif mkuu mpya wa MINUSMA:Ban

Mahamat Saleh Annafif mkuu mpya wa MINUSMA:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-Moon leo ametangaza uteuzi wa Mahamat Saleh Annadif wa Chad kuwa mwakilishi wake maalumu na pia kuwa mkuu wa mpango wa Umoja nchini Mali (MINUSMA). Bwana Annadif anachukua nafasi ya Mongi Hamdi wa Tunisia, ambaye atahitimisha muda wake Januari 14 mwaka 2016. Katibu Mkuu amemshukuru bwana Hamdi kwa huduma na uongozi bora MINUSMA.

Bwana Annadif ambaye ataingia katika wadhifa huu mpya na uzoefu mkubwa wa kitaifa na kimataifa amewahi kuwa waziri wa mambo ya nje wa Chad kati ya 1997-2012 ameshika nyadhifa mbalimbali serikalini ikiwepo katibu mkuu wa Rais.

Pia amewahi kuwa mwakilishi wa kudumu wa tume ya Muungano wa Afrika kwenye jumuiya ya Muungano wa Ulaya kuanzia mwaka 2006 hadi 2010. Na wakati wote wa utendaji wake wa kazi ameshiriki michakato mbalimbali ya Amani Afrika ikiwemo Niger, Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR na Sudan.

Na kuanzia mwaka 2012 hadi 2014 amekuwa mwakilishi maalumu wa Muungano wa Afrika na mkuu wa mpango wa kulinda Amani wa Muungano wa Afrika nchini Somalia AMISOM.