Mkuu wa UNISDR akaribisha siku ya kimataifa ya kelimisha kuhusu tsunami:

23 Disemba 2015

Uamuzi wa baraza kuu la Umoja wa mataifa kutambua na kutenga siku ambayo itachagiza na kuelimisha umma kuhusu tsunami utasaidia kuweka msukumo katika njia za kupunguza majanga ya asili nay ale yanayosababishwa na binadamu.

Hiyo ni tathimini ya mkuu wa ofisi ya Umoja wa mataifa ya upunguzaji wa hatari ya majanga UNISDRbi Margareta Wahlström.

Jumanne wiki hii baraza kuu limepitisha azimio la kuifanya tarehe 5 Novemba kila mwaka kuwa ni siku ya kimataifa ya uelimishaji kuhusu Tsunami.

Katika taarifa yake Bi Wahlström amesema kuelimisha jamii kuhusu majanga kutasaidia kuokoa maisha ya watu na mali zao. Anakumbuka kwamba tsunami yam waka 2004 kwenye bahari ya Hindi ambayo iliuwa Zaidi ya watu 200,000 iliibua dhamira za kisiasa za kupunguza hatari ya majanga na hasara.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter