Misafara ya kurejea nyumbani Cote D'Ivoire yaanza huko Liberia..

Misafara ya kurejea nyumbani Cote D'Ivoire yaanza huko Liberia..

Nchini Liberia, kazi ya kuwarejesha nyumbani kwa hiari wakimbizi wa Cote D'Ivoire waliokuwa wakiishi nchini humo imeanza tena baada ya kusitishwa kwa zaidi ya mwaka mmoja. Kuanza kurejea kwa wakimbizi hao kunafuatia mazungumzo ya utatu kati ya serikali za nchi mbili hizo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR yaliyofanyika mwezi Machi mwaka huu na kuridhia kuanza tena kwa mpango huo. Je nini kimefanyika na mipango ya baadaye ni ipi? Assumpta Massoi anafafanua zaidi kwenye makala hii.