Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchaguzi CAR uwe wa Amani, huru na wa haki: Bocoum

Uchaguzi CAR uwe wa Amani, huru na wa haki: Bocoum

Mtaalamu huru wa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR Marie-Thérèse Keita Bocoum, amewapongeza takribani milioni mbili waliojiandikisha kupiga kura kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge.

Mtaalamu huyo amewachagiza raia wa nchi hiyo kushiriki kura hiyo muhimu ambayo itafanyika Jumapili Desemba 27, na kuwataka waepukane na vitendo vyovyote vya uchochezi na ghasia.

(SAUTI YA Marie-Thérèse Keita Bocoum)

“Natoa wito hasa kwa serikali ya sasa na Umoja wa Mataifa ikiwemo MINUSCA kufanya kila juhudi kuzuia aina yoyote ya ghasia, kuwazuia watu wanaopendelea Zaidi silaha, kufanya kila njia kuzuia madhara na kuwafikisha mbele ya sheria wale watakaotekelweza vitendo vya ghasia ili haki itendeke ili tusiwe tena na vitendo vya madhara kwa watu , lakini pia watu waweze kwenda vituoni kupiga kura na kwamba wagombea wahitimishe kampeni zao kwa utulivu na sauti ya demokrasia ndio itawale.”