Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yahaha kusaidia wakimbizi wa ndani Ukraine

UNHCR yahaha kusaidia wakimbizi wa ndani Ukraine

Nchini Ukraine, msimu wa baridi ulioanza hivi karibuni unathiri zaidi maisha ya watu milioni 2 waliolazimika kuhama makwao kwa sababu ya mapigano nchini humo.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR limesema kwenye taarifa iliyotolewa leo kwamba takriban watu 800,000 wanaishi kwenye mazingira magumu kwenye maeneo ya mapigano, wakihitaji huduma za msingi ikiwemo huduma ya kupasha nyumba zao, na nguo za kujisitiri na baridi kali.

UNHCR imeeleza kuwa imeshapeleka tani 1,000 ya vifaa vya kibinadamu na misaada ya dharura kwenye maeneo yaliyoathirika zaidi, licha ya changamoto kubwa katika kufikisha misaada hiyo.