Wakimbizi na wahamiaji kuongezeka 2016: UNHCR

23 Disemba 2015

Shirika la Umoja wa Mataiafa la Wakimbizi(UNHCR), limesema janga la wakimbizi litaendelea mwaka ujao kwa kuwa suluhu la migogoro mingi mathalani Syria haionekani kuzaa matunda na hivyo hitaji la misaada ya kibinadamu ni dhahiri linaongezeka.

Katika mahojiano na idhaa hii msemaji wa UNHCR Adrian Edwards amesema wahamiaji na wakimbizi wataongezeka mwaka 2016 hususani barani Ulaya na kwamba kinachotia hofu zaidi ni kuwa idadi hiyo hailingani kabisa na mwitikio wa usaidizi kwa kundi hilo.

Msemaji huyo wa UNHCR amesema kile ambacho shirika lake lionafanya.

(SAUTI ya Adrian)

‘‘Tayari kwa sasa kama tulivyosema hapo awali, tunaona visingizio au kuonewa kwa watu wanaokimbia migogoro mikali, na hilo ni tatizo kubwa kwani halifanyi lolote katika kuleta suluhisho kwa tatizo hili, na hii ni tishio lingine ambalo llitatubidi tukabiliane nalo mwaka 2016 katika mazingira haya ambayo wakimbizi wanazidi kutumiwa kama mtaji wa kisiasa’’

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter