Skip to main content

MONUSCO na Radio OKAPI kuelimisha jamii kuhusu ukimwi.

MONUSCO na Radio OKAPI kuelimisha jamii kuhusu ukimwi.

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, bado ukimwi ni janga linalotishia afya ya umma. Kwa mujibu wa Radio Okapi ikitaja ripoti ya asasi isiyoya kiserikali ya Médecins sans Frontières, watu 450,000 wanaishi na virusi vya ukimwi na miongoni mwao asilimia 80 hawana fursa au uwezo wa kupatiwa matibabu aina ya ARV.

Katika mkakati wa kutokomeza ugonjwa wa ukimwi nchini DRC, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC MONUSCO pamoja na Radio OKAPI zimeshirikiana na kutunga wimbo wa kuelimisha jamii.

Kulikoni? ungana na Flora Nducha kwenye makala hii.