Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti zamulika ukwepaji sheria Mali

Ripoti zamulika ukwepaji sheria Mali

Ripoti mbili za Umoja wa Mataifa zilizotolewa leo zinaonyesha umuhimu wa kukomesha ukwepaji sheria kwa vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu vilivyofanyika mwaka 2014 na 2015 nchini Mali.

Ripoti ya kwanza iliyotolewa kwa pamoja na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali, MINUSMA na Kamisheni Kuu ya haki za Binadamu, imechunguza uhalifu uliofanyika na waasi na jeshi la Mali kwenye eneo la Kidal mwaka 2014, ikisema baadhi ya vitendo vilivyochunguza vilikuwa sawa na uhalifu wa kivita.

Ripoti ya pili imechunguza uhalifu uliofanyika kwenye eneo la Gao mwezi Mei mwaka 2015, ikionyesha kwamba hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa na serikali ya Mali ili kulinda raia na kuchunguza uhalifu huo.

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu Zeid Ra 'ad Al Hussein amesema ni lazima kuwatendea haki wahanga wa matukio hayo ili kujenga amani na maridhiano nchini Mali.