Skip to main content

MONUSCO yateketeza kambi ya ADF Beni

MONUSCO yateketeza kambi ya ADF Beni

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC umetangaza kushambulia kambi ya waasi wa ADF iliyoko karibu ya Eringeti, kwenye maeneo ya Beni, Kivu Kaskazini.

Hii ni kwa mujibu wa Naibu Msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq ambaye amesema hayo akizungumza leo na waandishi wa habari mjini New York Marekani, akieleza kwamba shambulio hilo limetekelezwa tarehe 19 Disemba na helikopta za mashambulizi za MONUSCO.

Aidha amesema kwamba operesheni hiyo imeandaliwa kwa ushirikiano na jeshi la kitaifa la DRC, FARDC.

Bwana Haq amesema kwamba MONUSCO inaendelea kutathmini matokeo ya operesheni hiyo.