Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lajadili ugaidi Afghanistan, lapitisha azimio kuukabili

Baraza la Usalama lajadili ugaidi Afghanistan, lapitisha azimio kuukabili

Wajumbe wa Baraza la Usalama wa Umoja wa Mataifa, leo kwa kauli moja wamepitisha azimio la kukabiliana na vitendo vya kigaidi nchini Afghanistan, wakati wakikutana kujadili kuhusu vitendo hivyo na tishio lake kwa amani na usalama kimataifa. Taarifa kamili na Amina Hassan.

(TAARIFA YA AMINA)

Acts

Ni Balozi Samantha Power wa Marekani akitangaza matokeo ya kura iliyopitisha azimio linalozitaka nchi zote zichukue hatua za kuzuia pesa na mali za watu au vikundi vinavyotishia amani na usalama nchini Afghanistan kwa vitendo vyao vya kigaidi.

Aidha, azimio hilo linazitaka nchi zizuie safari za watu na vikundi hivyo vya kigaidi, pamoja na usafirishaji au uuzaji wa silaha kwa vikundi hivyo.

Baada ya kupitishwa azimio hilo, Baraza la Usalama limehutubiwa na Mwakilishi wa Katibu Mkuu na Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa Afghanistan, UNAMA, Nicholas Haysom, akielezea hali ilivyo