UNSOM yalaani mashambulizi ya kigaidi Mogadishu

UNSOM yalaani mashambulizi ya kigaidi Mogadishu

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Nicolas Kay amelaani vikali shambulizi la Jumamosi kwenye mji mkuu Mogadishu. Taarifa kamili na Joshua Mmali.

(Taarifa ya Joshua)

Shambulio lililotokea baada ya gari lililokuwa na bomu kulipuka katika moja ya barabara yenye shughuli nyingi mjini humo na kusababisha vifo vya watu kadhaa na wengine wengi kujeruhiwa.

Kikundi cha kigaidi cha Al-Shabab kimekiri kuhusika na shambulio hilo ambapo Bwana Kay amesema matumizi ya mbinu hizo za kushambulia hovyo raia wanaokuwa kwenye shughuli zao za kila siku ni ukatili na uhalifu unaotia aibu.

Bwana Kay ametuma rambirambi kwa familia za wafiwa na marafiki zao huku akisisitiza azma ya Umoja wa Mataifa ya kuendelea kusaidia Somalia na ukanda husiak katika kujenga usalama na utulivu.