Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hungary yatakiwa kujizuia na sera na vitendo vinavyochagiza chuki na kutovumiliana

Hungary yatakiwa kujizuia na sera na vitendo vinavyochagiza chuki na kutovumiliana

Shirika la Umoja wa mataifa UNHCR, baraza la Muungano wa Ulaya na ofisi kwa ajili ya taasisi za demokrasia na haki za binadamu (ODHIR) zimeitaka serikali ya Hungary kujizuia na sera na vitendo vinavyochagiza kutovumiliana, hofu na kuchochea chuki dhidi ya wakimbizi na wahamiaji.

Mashirika hayo yameungana katika kauali hiyo ya pamoja na kutoa wito kwa serikali ya kupitisha roho ya ubinadamu nia ya kuwasaidia wale ambao wamelazimika kukimbia nchi na kwa sasa wanasaka usalama katika bara Ulaya. William Spindler ni afisa wa UNHCR.

(SAUTI YA SPINDLER)

Serikali ya Hungsry imezindua kampeni mpya kwa umma mwezi huu wa Desemba inayowaonyesha wale wanaokimbia vita na migogoro kama wahalifu, wavamizi na magaidi kutokana na imani zao za kidini na maeneo wanakotoka.