Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mila potofu zaathiri haki za binadamu Liberia

Mila potofu zaathiri haki za binadamu Liberia

Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo inaonyesha jinsi badhi ya mila na utamaduni unavyoathiri haki za binadamu nchini Liberia. Taarifa zaidi na Grace Kaneyia.

(Taarifa ya Grace)

Ukeketaji, uchawi na vyama vya kisiri ni miongoni mwa mila zilizobainika kupitia utafiti uliofanyika kati ya mwezi Januari mwaka 2012 na Septemba mwaka 2015.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Haki za Binadamu inasema kwamba wanawake, wazee na watoto ndio wahanga wa mila hizo potofu na mara nyingi watekelezaji wao hukwepa sheria.

Aidha ripoti imemulika mauaji ya kimila ambayo idadi yao inatarajiwa kuongezeka ifikapo uchaguzi mkuu wa mwaka 2017.

Hatimaye ripoti ambayo imeandaliwa kwa ushirikiano na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo imesisitiza umuhimu wa kuimarisha mamlaka za serikali na mifumo ya sheria nchini humo ili kupambana na uhalifu huo.